Rashford ajifananisha na Ronaldo baada ya kufunga goli la kichwa dhidi ya Newcastle “Sijamfikia Ronaldo kuruka lakini nalifanyia kazi”
Rashford ajifananisha na Ronaldo baada ya kufunga goli la kichwa dhidi ya Newcastle "Sijamfikia Ronaldo kuruka lakini nalifanyia kazi"
Mchezaji wa Mnachester United na timu ya taifa ya Uingereza Marcos Rashford ameamua kutoa ya moyoni na hisia zake baada ya kufunga goli la kichwa dhidi ya Newcstle United. Mchezo huo ambao ulichezwa katika uwanja wa Old Trfford Manchester United walifanikiwa kupata ushindi wa goli 4-1 liccha ya kutoka nyuma baada ya Newcastle kutangulia kupata goli.
Newcatle walifungua milango ya magoli mnamo dakika ya 17 tu ya mchezo baada ya Matty Logstaff kufunga goli zuri kabisa, Licha ya Logstaff kufunga goli hilo hii inakuwa mara ya pili baada ya kuifunga Manchester katika mchezo wa kwanza ambapo United walipoteza ugenini dhid ya Newcatle na hii kikawa kama kisasi kwa United, Dakika ya 24 Anthony Martial alirudi mchezoni baada ya kuipatia United goli la kusawazisha lakini dakika ya 36 kijana machachari mwenye umri wa miaka 18 Mason Greenwood aliipatia United goli la 2 lakini kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika Marcos Rashford aliipatia United goli la 3 dakika ya 41 kwa kichwa na Martial kufunga ukurasa mano dakika ya 51.
Ushindi huo wa United unaifanya kusogea hadi nafasi ya 7 wakiwa na alama 28 kwenye msimamo wa ligi, Goli la Rashford dakika ya 41 ndio ambalo limemfanya kuongea maneno yote hayo na kujihisi anataka kumfikia Cristiano Ronaldo aina yake ya ufungaji.
Ikumbukwe hii sio mara ya kwanza Rashford kufananishwa na Ronaldo kwani katika mchezo wa Chelsea dhidi ya United katika kombe la Carabao alifunga goli la freekick ambalo mchezaji mwenzake wa United raia wa Sweden Lindelof alisema kuwa hili goli kama nishawahi kuliona kabla huku akipost picha ya Ronaldo akifunga goli kama hilo.
Udakumania ™
©2019.
0 Comments