Viongozi wa serikali ya Somalia na Umoja wa Mataifa (UN) wamelaani vikali shambulizi la kigaidi lililotokea Mogadishu, Somalia na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 80 na wengine 149 kujeruhiwa hadi sasa.
Msemaji wa serikali ya Somalia Ismael Mukhtar Omar amethibitisha idadi ya vifo hivyo vilivyotokana na lori lililotegwa bomu kulipuka katika kituo cha ukaguzi wa usalama katika barabara ya Afgoye iliyopo viunga vya Mogadishu.
Kwa mujibu wa Bw. Omar, miongoni mwa watu waliokufa wamo wanafunzi takriban 15 wa chuo kikuu cha Banadir.
Afisa wa polisi aliyepo kwenye eneo la tukio amesema mlipuko huo uliolenga ofisi ya kodi ya mapato ulitokea ghafla wakati polisi wanakagua gari zinazopita barabarani na kusababisha vifo na uharibifu mkubwa.
Udakumania ™
©2019
0 Comments