Virusi vya Corona
Virusi vya Corona (kwa Kiingereza: Coronavirus) ni kundi la virusivinavyoweza kusababisha magonjwakwa wanyama (mamalia na ndege) lakini pia kwa binadamu[1]. Inaaminiwa ni aina ya virusi vilivyohama kutoka kwa wanyama na kuathiri binadamu pia.
Virusi vya Corona vipo vya aina mbalimbali, zikiwemo 229E, NL63, OC43, HKU1 na SARS-Cov-2 [2][3].
Tabia za pamoja
Virusi vya corona huwa na uwezo wa kubadilika na aina nyingi husababisha magonjwa yasiyo hatari sana upande wa binadamu. Kudhoofika kwa mwili kutokana na mashambulio ya virusi kunafungua milango kwa bakteria wabaya kukuvamia na kusababisha maambukizo ya mfumo wa upumuo, kama mafua au homa ya mafua(influenza), yanayoishia kwa kawaida baada ya siku kadhaa, lakini kuna pia maambukizo ya hatari kama nimoniainayoweza kusababisha kifo. Hivyo inatakiwa watu wapunguze kutumia kwa pamoja vitu hatarishi kama vile vya ncha kali[4].
Hadi sasa hakuna chanjo au dawa ya kudhibiti virusi vya aina hii. Kwa hiyo uponyaji hutegemea mara kwa mara nguvu ya kinga mwilini cha kila mtu. Hii inamaanisha virusi hivi huleta hatari hasa kwa watu wenye kinga cha mwili kilichodhoofishwa.
Aina hizo za virusi zina uwezo wa kubadilika, miaka ya nyuma ulikuwa na mabadiliko kadhaa yaliyosababisha vifo vya watu na kuenea haraka kimataifa, hivyo kusababisha hofu za epidemiki au hata pandemia.
SARS
SARS (Severe acute respiratory syndrome)ulikuwa ugonjwa sugu wa mfumo wa upumuo uliosababishwa na virusi vya corona aina ya SARS-CoV. Uliripotiwa mara ya kwanza huko Asia kwenye Februari 2003 ukaendelea kusambaa katika miezi iliyofuata katika nchi zaidi ya 20 katika AmerikaUlaya na Asia hadi kwisha. Ugonjwa ulianza kuonekana kwa homa juu ya  38, maumivu ya kichwana kujisika dhaifu. Asilimia 10-20 za wagonjwa walihara. Wengi walioambukizwa waliendelea hata kupata nimonia. Kulikuwa na taarifa za watu 8,098 walioambukizwa, na 774 walifariki katika nchi 17[5], wengi wao nchini China. [6]
SARS haijatokea tena tangu mwaka 2004.
Covid-19 (2019 Novel Coronavirus SARS-Cov-2)
Kwa habari za undani zaidi kuhusu uenezaji wa ugonjwa wa Covid-19 tazama hapa (Kiingereza)
Mwisho wa mwaka 2019 lilitokea badiliko jipya la virusi vya corona lililotambuliwa mara ya kwanza mjiniWuhanChina[7] Serikali ya China inalaumiwa kwa kujaribu kuficha ugunduzi huo kwa maagizo yalitolewa tarehe 2 Januari 2020.
Aina hiyo ya virusi vya corona iliitwa mwanzoni 2019 Novel Coronavirus (2019-nCoV) na hatimaye ikapewa jina la SARS-Cov-2, na ugonjwa unaosababishwa nayo Covid-19 [8]. Usambazaji wake ulionekana kuanza kutokana na virusi vya wanyama vilivyofikia binadamu. Magonjwa ya aina hiyo huitwa zuonosia (zoonotic disease).
Wagonjwa walionyesha matatizo kwenye njia ya upumuo; wengine waliathiriwa kidogo tu, lakini wengine waligonjeka vibaya hadi kufa. Dalili zilizotambuliwa hadi mwisho wa Januari 2020 ni pamoja na homa, kukohoa na ugumu wa kuvuta pumzi. Inaonekana dalili za ugonjwa zinaweza kuanza takriban siku 2 hadi 14 baada ya kuambukizwa. Walio hatarini zaidi ni watu waliodhoofishwa na magonjwa mengine au wenye mfumo dhaifu wa kinga mwilini kwa sababu nyingine, kwa mfano umri mkubwa.
Hadi mwisho wa Januari 2020 takriban watu 10,000 waliambukizwa, idadi ya vifo ilikuwa mnamo 200. Virusi vilienea hadi nchi nyingine kwa njia ya abiria wa ndegeza kimataifa. Wakazi wa Wuhan na miji mingine ya China yenye wagonjwa wamekataliwa kuondoka kwao baada ya hali ya karantini kutangazwa.[9].
Katikati ya Februari 2020 maswali mengi kuhusu virusi hivi vilibaki bila jibu, lakini Shirika la Afya Duniani lilitoa tathmini kuwa[10]
  • zaidi ya asilimia 80 za wagonjwa huonekana kuwa na ugonjwa mwepesi, wanapona
  • kati ya asilimia za wagonjwa kuna maambukizi mazito yanayosababisha matatizo ya kupumua, hata nimonia, na asilimia 15 kudai walazwe hospitalini
  • takriban asilimia 5 huwa na magonjwa hatari
  • mnamo asilimia 2 hufa; hatari ya kifo inapatikana hasa kwa wazee, kuna mfano michache ya watoto. Baadaye imeonekana kwamba kiwango cha vifosi kubwa vile, labda kati ya % 0.5 hadi 1 lakini si rahisi kutaja kiwango kwa uhakika kwa sababu wengi walioambukizwa hawajulikani.
  • utafiti wa ziada bado unahitajika
  • kuna dalili kwamba virusi vya Covid-19vinaweza kudumu hadi siku 8 kwenye uso wa kitu kilichoguswa na mgonjwa na bado kusababisha maambukizi
Uenezi wa Covid-19 nje ya China
Uenezaji wa virusi vya SARS-Covid-19 duniani (ramani inasahiishwa kila siku)
Idadi ya watu waliothibitishwa kuwa na maambukizi
  zaidi ya 10,000
  1,000–9,999
  100–999
  10–99
  1–9
(Tarehe 16 Machi mtu wa kwanza alipatikana nchini Tanzania)
Katika Februari 2019 virusi viliendelea kuenea nje ya China, kupitia watu waliosafiri baina ya China na nchi nyingine. Tabia ya virusi kutosababisha ugonjwa mkali kwa wengi ilikuwa msingi kwa uenezaji usiotambuliwa mwanzoni hadi kufikia watu waliogonjeka vibaya. Milipuko ya kwanza ilionekana katika Iran[11]Korea Kusini[12] na Italia[13]ambako serikali zilitangaza hali ya karantini kwa maeneo kadhaa. Kufikia mwisho wa mwezi huo, wagonjwa wa nchi nyingine kwa pamoja walikuwa wamezidi wale wa China.
Katika Machi 2020 idadi ya maambukizi mapya ilipungua nchini China na Korea Kusini lakini iliongezeka Ulaya na kuanza kusambaa Marekani. Katika Ulaya Italia ilikuwa nchi iliyoathiriwa vibaya zaidi; serikali ilifunga shule zote pamoja na maduka yasiyo ya chakulas na dawa na kupiga marufuku mikusanyiko yote, ikiwemo ile ya ibada. Hatua kama hizo zilichukuliwa pia katika nchi nyingine. Katika Asia ya Magharibi nchi iliyoathiriwa vibaya zaidi ni Iran.
Kwa jumla si rahisi kupata picha kamili ya uenezi halisi wa virusi hivi. Ilhali dalili za ugonjwa zinafanana na mafua ya kawaida na kifua kikuu, inawezekana mara nyingi maambukizi hayakutambuliwa. Kwa sababu hiyo makadirio ya asilimia ya watu wanaokufa yanatofautiana kati ya nchi na nchi.
Tarehe 11 Machi 2020 Shirika la Afya Duniani ilitamka uenezi wa virusi umefikia ngazi ya pandemia, yaani epidemia (mlipuko) katika nchi nyingi za dunia[14].
Katikati ya mwezi Machi 2020 idadi ya wagonjwa iliongezeka sana katika nchi za Ulaya. Marekani ilizuia wasafiri kutoka Ulaya kuingia. Nchi mbalimbali, pamoja na Ujerumani, zilianza kufunga shule na kukataza mikutano yote yaliyolenga zaidi ya watu 100-500, kwa hiyo kufunga mechi za mpira wa miguu au michezo mingine, pamoja na hoteli na sinema. Kampuni mbalimbali ziliamuru wafanyakazi kukaa nyumbani na kutekeleza shughuli kupitia kompyuta pekee. Tarehe 14 Machi Denmark na Poland zilifunga mipaka kwa wote wasio raia wao, kwa kuamuru raia waliorudi wapaswe kukaa karantini wiki 2.
Kwa jumla serikali zilitangaza kwamba asilimia kubwa ya wananchi wataambukizwa zikiona changamoto kuchelewesha mchakato wa maambukizi ili wale wataokuwa wagonjwa sana wasijitokeze mara moja lakini polepole ili waweze kuhudumiwa hospitalini.
Kufikia tarehe 19 Machi nchi 170 zilikuwa na mgonjwa walau mmoja. Jumla ilifikia 227,000 na vifo 9,300 kati nchi 40. Ulaya ilikuwa imezidi China kwa wingi wa vifo. Tarehe 18 Machi nchini Italia walifariki watu 475, kuliko siku yoyote ya China.
Afrika
Mwanzoni mwa Machi 2020 hakukuwa na taarifa ya maambukizi mengi ndani ya Afrika. Wataalamu walijadiliana kama hilo ni jambo linalotokana na kukosa vifaa vya kupima na kutambua ugonjwa, au kama kuna sababu ya ugonjwa kutoenea katika Afrika. Wagonjwa wengi waliotambuliwa kusini kwa Sahara ni wasafiri waliofika kutoka nchi za nje.
Hadi 12 Machi wagonjwa walithibitishwa hasa katika Afrika KaskaziniMisriwagonjwa 67 (1 alifariki), Algeria 20 (0), Moroko 6 (1) na Tunisia 7 (0). Upande wa kusini wa Sahara taarifa zilipatikana hasa kutoka Afrika Kusini walipotambulia wagonjwa 17 (0), wengi wao watu waliorudi kutoka safari za Italia. Togoilikuwa na mgonjwa 1 (0) aliyethibitishwa, Senegal 4 (0), Nigeria 2 (0), Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo 1 (0), Kamerun 2 (0), Burkina Faso 2 (0)[15]
Tarehe 15 Machi jioni mtu wa kwanza alithibitishwa Tanzania akiambukizwa; hadi tarehe 19 idadi ilifikia waambukizwa 6.[16] Wote waliambukizwa nje ya nchi wakagundulika baada ya kufika Tanzania.
Ushauri wa kujikinga dhidi ya maambukizi
Maambukizi husambaa hasa kwa majimaji ya mwilini, kama matone madogo ya mate au chafya; mtu aliyeambukizwa atakuwa na virusi kwenye mikono yake akigusa pua au mdomo. Inawezekana mtu aliyeambukizwa asionyeshe dalili za ugonjwa bado lakini anaweza kupitisha virusi tayari.
Unashauriwa:
  • kunawa mikono mara kwa mara kwa angalau sekunde 20 kwa maji na sabuni. Ukiwa nayo tumia dawa yenye alikoholi (si chini ya asilimia 60) kusafisha mikono.
  • usiguse macho, pua na midomo kwa mikono kama hujanawa
  • epuka kuwa karibu sana na wagonjwa, tumia barakoa ya kinga ukimhudumia mgonjwa
  • ikiwezekana epuka kuingia katika msongamano mkubwa wa watu maana wenye virusi hawaonekani kirahisi.
  • kaa nyumbani ukiwa mgonjwa (ugonjwa wowote - maana kinga yako ni dhaifu katika hali hii)
  • tembea na karatasi za shashi (kama huna, hata karatasi ya choo / toilet paper) uitumie ukikohoa au kupiga chafya, halafu uitupe mahali pa takataka
  • safisha mara kwa mara vitu unavyovigusa (vikiwa pamoja na kikombemezadawatisimu yako)[17]