Muda mchache baada ya Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli kumlipia faini ya  milioni 38 kati ya 48 mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa ameibuka hasimu wake Msanii wa bongo movie steve nyerere na kumshukuru Rais kwa uamuzi huo huku akisema kuwa alikosa raha kumuona kidume cha mbegu kipo ndani.

Kupitia akaunti yake ya instagram Steve Nyerere  alipost picha ya Rais Magufuli akishikana mikono na Mchungaji msigwa  na kushangaa Du huku akicheka sana.

Hakuishia hapo Steve aliandika;

Nimefurahi sana hakika Mh RAIS MAGUFURI Niseme asante sana, Maana Nilikosa raha sana kumwona KIDUME CHA MBEGU kipo ndani hata 40 hakina, Iyo milioni 2 Basi maliza sio kusumbua wananchi tena hahahahahahahahahah