Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) na Mchungaji wa Kanisa la Mlima wa Moto (Mikocheni B Assemblies of God ) Mchungaji Dk. Getrude Lwakatare amefariki dunia Alfajiri ya leo. Mtoto wa amarehemu amethibitisha kifo.

Mtoto wa Marehemu Mama Rwakatare, Mutta Rwakatare amethibitisha kwa kusema

"Ni bahati mbaya imetokea asubuhi ya leo saa 11 kasoro, alikuwa na matatizo ya moyo, jana tulimkimbiza Hospitali lakini bahati mbaya imetokea, tupo katika hatua ya kuangalia namna gani tutafanya ili tuweze kumpumzisha mama yetu" amesema Muta.