Kabla ya picha ya George Floyd kuangushwa na kukabwa chini ya miguu ya polisi na hivyo kusababisha chuki, hasira na maandamano nchini Marekani, historia ya maisha yake ilikuaje?

Floyd amepoteza maisha. Lakini katika ukuaji wake alikuwa anacheza soka nchini Marekani kwenye klabu ya Yates High School Lions katika mji wa Houston mwaka 1992.

Mwaka 2007 alikamatwa kwa kosa la kupora na mahakama iliamuru kufungwa miaka mitano jela.

Hata hivyo Floyd, 46, alikuwa anajulikana katika mji wa Minneapolis ambapo hadi umauti unamkuta Mei 25, 2020, ni miongoni mwa watu wa Marekani ambao walikuwa wanatafuta tonge la kila siku kwa kukabiliana na changamoto za maisha ya hapa na pale.

Kifo chake kimesababisha huduma za umma, za kiafya kuwa hafifu hata janga la kiuchumi kwa Wamarekani kutokana na maandano yanayoendelea nchini humo.

Kwa wakazi wa Houston, Texas, ambako Floyd alikulia katika miji ambayo ina idadi kubwa ya watu wenye asilia ya Afrika, Kusini mwa jiji hilo la Minneapolis wanafahamika kwa maisha yao ya kawaida ya kati.

Majina makubwa katika tasnia ya muziki nchini Marekani yameanzia huko, msanii Beyoncé amekulia katika mji huo, Drake mwanahip-hop raia wa Canada pia amekulia maeneo hayo ambayo yanaelezwa kuwa na watu wenye mawazo ya muziki wenye utamaduni wa hip-hop.

Licha ya majina makubwa kutokea huko bado kuna changamoto kubwa kama umasikini, ubaguzi wa rangi na ukosefu wa usawa kiuchumi umekuwa siri ya wakazi katika mji huo, na miji mingine nchini Marekani.

"Muda wote nikiona mtu ambaye sio mwenyeji wa maeneo haya huwa namwambia kuwa hakuna umasikini kama ule".

"Kuna shida kubwa, ni mji wa kihuni haswa" alisema Ronnie Lillard ambaye alikuwa rafiki wa karibu wa George Floyd alipoongea na BBC.

"Bado watu wanaishi kwa shida, milio ya bunduki kawaida kabisa huku. Kuishi huku ni vigumu kukwepa matukio kama hayo" aliongeza Lillard ambaye anaimba mziki aina ya hip-hop alitumia jina la Reconcile.

George Floyd on a protester's T-shirt

Floyd alikuwa anajulikana sana katika shughuli za uratibu wa majengo, pia alikuwa kama muandaaji wa tofali za kujengea majengo hayo na wenzake kama akina Coney Homes.

Alikuwa ni mtu mwenye miraba minne akiwa na futi sita na nchi sita, rafiki zake waliokuwa nae utotoni wanamwelezea kama mwanamume mkamilifu zaidi kwa namna alivyojengeka akimudu vyema soka la Marekani na mpira wa kikapu.

"Tulikuwa na miaka 12 pekee lakini yeye alionekana mkubwa kwetu, alikuwa na mguu wenye urefu wa futi sita, rafiki yake mmoja wa utotoni alimwelezea Floyd anayefahamika kwa jina la Jonathan Veal, "sikuwai kumuona mtu mrefu kama yeye" aliongeza.

Katika timu ya John Yates High School, alikuwa akivalia jezi nambari 88 kipindi hicho anasakata kabumbu ya America, lakini baadae alionekana angefaa kucheza mpira wa kikapu katika timu ya chuo ya Florida ya Kusini ambao alikuja kuhamia huko mwaka 1993 hadi 1995, kwa mjibu wa CNN.

Alirudi tena Texas kwenye Chuo cha A&M , Kingsville hata hivyo hakumalizia masomo yake ngazi ya Chuo.

Maisha ya Floyd yalibadilika ghafla mwaka 2007 baada ya kukamatwa kwa wizi na madai ya matumizi ya madawa ya kulevya ambapo baadae alitupwa jela miaka mitano.

Baada ya kutumikia kifungo alitoka na kuanza kijihusisha na shughuli za serikali ya mitaa na uokaji katika mji wa Houston, akawa karibu na watu akijitahidi kuondoa dhana potofu dhidi yake.

Mwaka 2017 kuna video ilitoka na kusambaa kwenye mitandao ya kijamii iliyokuwa ina muonyesha ameshikiria silaha jambo lililopelekea kuongeza hamu ya watoto kurudi mapema nyumbani.

Familia yake mwake 2018 aliamia katika mji wa Minnesota baada ya kushawishiwa na marafiki zake na ndugu wa kiroho kupitia mpango wa kidini.

Christopher Harris, rafiki yake alisema (Floyd) alikuwa anatafuta mwanzo mpya wa maisha mapya na safari salama lakini imekatikia njiani".

"Alikuwa na furaha na mabadiliko aliyokuwa anayafanya, aliongeza.

Mchezaji mwezake waliyekuwa naye mwanzo ambaye hivi sasa ni mlinzi katika jeshi la uokoaji, sehemu ambayo anajulikana kama kaka mkubwa wa Floyd.

Kama ilivyo kwa Wamerakani wengi, popote pale penye upenyo wa fursa wa kufanya biashara au changamoto huchukuliwa kwa haraka.

Siku aliyokuwa anakamatwa alisema alikuwa anajaribu kununua sigara ndipo jaribio hilo liliposhindikana.

Hasira juu ya kifo cha Floyd kimewafanya wapingaji wengi kutoka maeneno tofauti tofauti duniani na hasa hapo hapo Marekani kupinga maonezi ambayo yamekuwa yakifanywa na polisi.

Marekani

Zaidi ya watu 1,600 wamekamatwa kutoka katika miji miwili na majimbo 15 kutokana na maandamano ya kupinga uonevu na mauaji ambayo yamekuwa yakifanyika nchini humo.

Bwana Lillard, ambaye alijitambulisha kama mtu wa amani amekuwa akiwahamasisha watu kuandamana ili haki za wanyonge kusikika katika maeneo mengi.

"Alikuwa na moyo mzuri kwa wote, alikuwa mtu wa watu, mwenye roho ya kusamehe kwa nini auawe?" Alisema.

"Nadhani kutokana na hili kuna kitu kimeongezeka kikubwa kuliko hata George Floyd," alizungumza Lillard alipokuwa anazungumzia maandamano hayo. "Kila mmoja ameumizwa kwa Mmarekani(aliyemuua) na haki ya Wamarekani wenyewe".