IDADI KUMBWA WA WANGONJWA YA RIPOTIWA JIMBO LA FLORIDA NDANI YA MASAA 24

Jimbo la Florid limekuwa na maandamano kutokana na masharti ya kutotoka nje
Maelezo ya picha,

Jimbo la Florid limekuwa na maandamano kutokana na masharti ya kutotoka nje

Jimbo la Florida limerekodi wagonjwa wapya 15,299 ndani ya saa 24-ikiwa ni robo ya idadi yote ya maambukizi ya kila siku nchini Marekani.

Jimbo hilo, lenye 7% pekee ya watu wote nchini Marekani, limepita rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na California.

Florida, ambayo ilianza kuondoa masharti yaliyowekwa ili kudhibiti maambukizi ya corona mwezi Mei, imeonekana kuwa hatarini kwa sababu ya shughuli za utalii na idadi ya wazee.

Florida pia imerekodi vifo 45 zaidi. Jimbo hilo linaweza kuwa katika nafasi ya nne duniani kwa idadi kubwa ya wagonjwa wapya kama ingekuwa nchi, kwa mujibu wa uchambuzi wa Reuters.

Zaidi ya hospitali 40 jimboni Florida zimesema kuwa vitengo vyao vya huduma kwa wagonjwa mahututi vimejaa.

Vyumba vya wagonjwa mahututi Florida vyakaribia kujaa

Idadi hii mpya ilitolewa siku moja baada ya kufunguliwa kwa eneo la kitalii la Walt Disney World huko Orlando, jimboni Florida, huku kukiwa na masharti ya kuhakikisha usalama wa kuvaa barakoa na matumizi ya vitakasa mikono.

Idadi ya maambukizi jimboni humo imeendelea kupanda ingawa Gavana Ron DeSantis wa chama cha Republican ameamuru kufungwa tena kwa vilabu vya pombe mwezi uliopita.

Mshauri wa juu wa Ikulu ya Marekani wa kikosikazi kinachoratibu mapambano dhidi ya virusi vya corona, Dkt Anthony Fauci, alikosoa kitendo cha kulegezwa kwa masharti ya kutotoka nje katika jimbo hilo, akisema kuwa data za maambukizi haziendani na hatua hiyo.

Bwana DeSantis pia amekataa suala la uvaaji barakoa kuwa la lazima.

Suala la barakoa limekuwa la kisiasa nchini Marekani, huku upinzani ukisema kuwa ni kuingilia uhuru wa mtu mmoja mmoja.

Idadai ya wagonjwa kila siku

Kumekuwa na maandamano dhidi ya amri ya uvaaji barakoa na hatua nyingine za kupambana na Covid-19 katika majimbo kadhaa.

Lakini siku ya Jumamosi, Rais Donald Trump alionekana akiwa amevaa barakoa hadharani kwa mara ya kwanza baada ya awali akionesha mashaka kuhusu umuhimu wa matumizi yake.

Alikuwa akitembelea hospitali ya kijeshi ya Walter Reed nje ya jiji la Washington, ambapo alikutana na wanajeshi waliojeruhiwa na wafanyakazi wa huduma za afya

Post a Comment

0 Comments