Kikundi cha Agner kimekuwa kikitambuliwa kama kampuni ya jeshi binafsi
Maelezo ya picha,

Kikundi cha Agner kimekuwa kikitambuliwa kama kampuni ya jeshi binafsi

Video zinazosambazwa hasa ndani ya Urusi na ripoti tofauti kutoka kwa timu za wachunguzi zinaonyesha mbinu za ukatili zinazotumiwa na wajumbe wa kikundi cha Wagner cha serikali ya Urusi.

Kama ilivyoonyeshwa katika ukanda wa video iliyochukuliwa ndani ya nyumba, kikundi hiki kiliwatesa na kuwakata viungo wahanga wanaowakamata.

Waandishi wa habari na wachambuzi ambao wamekua wakifuatilia shughuli zake wamekielezea kikundi hicho kama mtandao wa mamluki unaolinda maslahi ya serikali ya rais Vladimir ambacho kinaitwa aina fulani ya kikosi cha kijeshi "kisicho rasmi" kinachoilinda Urusi.

Wataalum hawa wanasema kikundi cha Wagner huendesha harakati zake nchini Syria na Libya, pamoja na Sudan na Jamuhuri ya Afrika ya Kati.

Uwepo wao katika eneo unakuwa na sababu inayofanana kwani wafuasi wa kundi hilo huwekwa katika maeneo ambako serikali ya Urusi ina maslahi yake.

Kwa mujibu wa Idhaa ya Kirusi ya BBC, serikali ya Kremlin ilikana uwepo kwa kikundi hicho na ikakana kuwa serikali ya Putin ina uhusiano na Wagner.

Mamluki

Kikundi cha Wagner kilipata umaarufu wake sana kwa kuunga mkono waasi wa Ukraine wanaoiunga mkono Urusi katika mzozo wa kijeshi wa Ukraine uliosababisha Urusi kutwaa eneo la Crimea mwaka 2014.

Tangu wakati huo, wale waliolitathmini wanalielezea kama jeshi ambalo linaweza kuwakodi mamluki na kuwatuma katika maeneo ya vita au kufanya matendo fulani kama vile kulinda eneo au kufanya mashambulio ya kulenga eneo fulani.

Kikundi cha Wagner kiliripotiwa kuhusika katika mzozo wa kivita wa Libya
Maelezo ya picha,

Kikundi cha Wagner kiliripotiwa kuhusika katika mzozo wa kivita wa Libya

Uhusiano na sera ya Putin

Kwa pamoja Mackinnon na Stronski wanaafiki kuwa uhusiano baina ya kikundi cha Wagner na serikali ya Vladimir Putin uko wazi.

"Wako tayari kupanua nafasi yao kama chombo cha siasa za Urusi nchini Libya na maeneo mengine muhimu ," anasema Paul Stronski.

Na anasema kwamba mshirika wa zamani wa Putin anayefahamika kama mmoja wa viongozi wa kikundi cha Wagner anadhihirisha kuwa Putin ana ushirika na kikundi hiki.

Kikundi cha Wagner kinapata ugumu, anasema mtafiti wa masuala ya sera za kigeni mwenye makao yake Washington, Amy Mackinnon, na kuongeza kuwa kuelezea na kubashiri operesheni za kikundi ni vigumu kutokana na tabia na utendaji wake.

"Tunaweza pia kusema ni kama kuwaweka katika mtandao unaofanya harakati za kutisha.

Wanaweza kukodi mamluki na kuwaajiri wapiganaji," aliiambia BBC mtaalamu huyo.

Mchambuzi huyo anatoa mfano wa kisa cha mateso na uvunjwaji wa viungo alivyofanyiwa mtu ambaye vyombo vya habari vya Urusi vilikuja kumtambua kama mhalifu wa jeshi la usalama la kibinafsi ambaye alikua mjenzi aliyetumiwa na kikundi cha Wagner .

Bwana Mackinnon anasema kuwa "mbinu hii ya hali ya juu " na "mbinu za ukatili ", zinazifanya serikali za magharibi kuwa na ugumu wa kuchukua hatua dhidi yao.

Vyombo vya habari vya Urusi na wachunguzi wameelezea kuwa vitendo vya wanachama wa kikundi cha Agner viko tafauti kabisa na vile vya vuguvugu la mrengo wa kulia linalopigania utaifa.

Wakati huohuo, Paul Stronski, Mkurugenzi wa mpango wa Urusi wa amani Carnegie Endowment for International Peace, ameiambia BBC kuwa makundi "hufanya kazi kama makundi mengi tofauti ya kivita, kwa kujifanya wauzaji wa silaha, watoaji wa mafunzo ya kijeshi kwa nchi walikoenda na wahudumu wa usalama" .

Wataalamu wanaeleza kuwa ingawa kikundi cha Group sio kikundi pekee cha kibinafsi chenye asili ya Urusi chenye mienendo hii, kinafahamika zaidi ya makundi mengine.

Makundi haya yanasemekana kuwa yanalinda sera ya Putin ya kigeni
Maelezo ya picha,

Makundi haya yanasemekana kuwa yanalinda sera ya Putin ya kigeni

Watafiti wanaonyesha kuwa Urusi ina uzoefu wa muda mrefu katika kutumia makundi haya katika miongo iliyopita.

"Kuna makundi mengine ya mamluki ambayo hutoa huduma," alisema.

Stronski anasema kuwa serikali ya Urusi imekuwa ikiongeza mara dufu juhudi zake katika nyakati tofauti ili kuhakikisha kwamba uhusiano wake na makundi haya ya wanamgambo hayafichuliwi na hivyo kuwekewa vikwazo vya kimataifa.

Amy Mackinnon, kwa upande wake, anasisitiza kwamba "hapana shaka " kwamba Wagner lina uhusiano na maslahi ya utawala wa rais Putin ingawa halitambuliwi na umma.

"Ninawachukuliwa kama sehemu ya Jeshi la Urusi," alisema.

Kwa upande wake serikali ya Putin inakanusha hilo.