Raia wa Sudan wameipongeza Wizara ya Haki na Sheria nchini humo kwa kutangaza mabadiliko kadhaa ya Sheria ikiwemo kupiga marufuku ukeketaji na kuzuia hukumu ya kifo kwa Watu wanaoasi Dini, mwanzoni Watu wanaoasi Dini walikuwa wanapewa hukumu ya kuuawa

Sheria nyingine iliyopongezwa ni ile ambayo Wanawake sasa hawatohitaji ruhusa tena kutoka kwa Wanaume au Walezi ili kusafiri na Watoto wao kama ilivyokuwa nyuma ambapo Mwanamke alilazimika hadi aombe ruhusa kwa Mwanaume ndipo aruhusiwe kusafiri na Mtoto wake.