A young man in a hoodie adminsters a swab test on himself

Madai ya kuwa vipimo vya corona vinaweza kusababishia watu madhara, yameenea katika mitandao ya kijamii.

Uchunguzi wa baadhi ya madai hayo ambayo yameshirikishwa katika mitandao ya kijamii.

Kipimo cha puani kinaweza kuharibu ubongo

Picha inayoonyesha mtu akipimwa corona puani 'swab test' imesambaa katika mitandao ya kijamii ya Facebook na Instagram ikiwa na madai kuwa kipimo hicho kinaweza kuleta kizuizi cha damu katika ubongo.

Wazo la kuwa kipimo hicho kinaweza kusababisha kizuizi cha damu katika ubongo, jambo ambalo halikueleweka hata kidogo kuhusu ufanyaji kazi wa kipimo hicho.

Ubongo una sehemu nyingi za kuulinda. Kwanza kabisa, fuvu la kichwa ni ulinzi tosha kwa ubongo na vilevile ubongo unalindwa na majimaji.

Mishipa ya damu ambayo inaenda kwenye ubongo, haiwezi kusababisha kuzuia damu kufika katika ubongo, wakati ikiruhusu vitu kama oksijeni na lishe .

Kipimo hicho cha kijiti cha pamba hakiwezi kuharibu tishu zozote au mfumo ambao upo na kufanya mishipa ishindwe kusukuma damu mpaka kwenye ubongo.

Post on social media claiming that the blood brain barrier is the spot where a coronavirus test using a nasal swab is carried out. We labelled it 'false'. Includes anatomical drawing of swab stick inside a nose.

"Kipimo hicho hakiwezi kufika katika kizuizi cha damu katika ubongo bila ya nguvu kubwa kutumika, maana kuna sehemu kadhaa ambazo zinalinda tishu na mifupa.

Hatujaona madhara yeyote ambayo yanasababishwa na kipimo cha corona tangu tumeanza kufanya vipimo hivi," alisema Dkt Liz Coulthard, mjumbe mtendaji wa 'British Neuroscience Association (BNA)'.

Mbinu ya upimaji wa virusi vya corona kwa kutumia kifaa hicho hakijaonyesha madhara hayo yanayotajwa.

Upatikanaji wa maambukizi kupitia koo na pua unatumiwa Uingereza kupima Covid-19 .

"Nimewapima wagonjwa wangu kwa kutumia mbinu hiyo hospitalini na vilevile kujipima mwenyewe kila wiki pamoja na watu ambao walijitolea kufanya jaribio la upimaji.

Haiwezekani kitu hicho ambacho kinaingizwa kwenye pua kwenda mbali kiasi hicho - unaweza kuhisi kuwashwa lakini hakuna maumivu yoyote," alisema Dkt Tom Wingfield kutoka shule ya tiba ya Liverpool.

Madai hayo ambayo yamejitokeza katika mtandao wa Facebook, katika kurasa za watu watano ambao wanaishi Marekani, Julai 6, madai hayo ni kama yanawataka watu wakatae kupimwa.

Madai hayo ni ya uongo.

Tumeona baadhi ya picha za grafiki ambazo ziko kwa lugha ya kirumi, kifaransa na kireno, huku maelfu ya watu wakiwa wameshiriki kutoa maoni.