by







Chama Cha Wakulima (Alliance for Africa Farmers Party) kimetoa wito kwa Wagombea waliokosa nafasi za Ubunge na Udiwani katika vyama vingine vya siasa wajiunge na chama chao

Wamesema wao bado wana nafasi nyingi zilizo wazi za Ubunge na Udiwani hivyo ni fursa kwa waliotaka kugombea kwani wataweza kutimiza ndoto zao za kugombea Uchaguzi Mkuu 2020

Aidha, AAFP imemteua Seif Maalim Seif kuwa mgombea urais kwa Tanzania huku Rashid Rai ambaye ni Katibu Mkuu wa chama akiteuliwa kuwa mgombea mwenza

Pia, kimemteua Said Sudi Said kuwa mgombea urais Zanzibar