Takwimu mpya nchini Ujerumani zinaonesha idadi ya watu wanaotafuta ulinzi kutokana na vita au mateso kutoka katika mataifa wanayotoka imeongezeka na kupindukia watu milioni 1.8 hadi mwishoni mwa mwaka uliopita.
Idadi hii mpya ya sasa inahusisha raia wa kigeni ambao wanawasili Ujerumani kutokana kuhitaji msaada wa kisheria, kisiasa na ya kibinaadam. Shirika hilo limesema hadi Desemba 31, takribani watu 266,000 walikuwa wakisubiri uamuzi wa mwisho wa maombi yao ya kutafuta hifadhi.
Idadi hiyo inatajwa kuwa ni pungufu ya asilimia 13 ikilinganishwa na kipindi kama hicho katika mwaka mmoja nyuma. Hata hivyo kiasi kingine cha watu milioni 1.36 wamepewa fursa ya kupata hifadhi
0 Comments