Idadi ya vifo kutokana na maambukizi ya virusi vya corona ulimwenguni yazidi kuongezeka.
Idadi ya vifo kutokana na mambukizi ya virusi vya corona ulimwenguni yazidi kuongezeka, watu 998 747 wamekwishafariki kutokana na virusi vya corona.
Idadi ya vifo kutokana na maambukizi ya virusi vya corona imeonegezeka ikilinganishwa na ilivyokuwa hapo awali.
Watu milioni 33,5 wameambukiwa virusi hivyo.
Idadi ya watu walioruhusiwa kuondoka hospitali imefikia watu milioni 24.4.
Nchini Marekani, watu 209 177 wamekwishafariki kutokana na maambukizi ya virusi vya corona huku watu milioni 7 wakiripotiwa kuwa na maambukizi ya virusi hivyo.
New York ndio eneo ambalo limeathirika kwa kiasi kikubwa na maambukizi ya virusi hivyo.
Nchini Uingereza , watu 34 wamefariki kutokana na maambukizi ya covid-19 ndani ya masaa 24.
Kutokana na vifo hivyo , idadi ya watu ambao wamefariki kutokana na maambukizi ya virusi hivyo imefikia watu 41 971.
Idadi ya watu walioambukiwa virusi hivyo imefikia watu laki 6.
Nchini Italia, watu 17 wamefariki ndani ya masaa 24 kutokana na maambukizi ya virusi vya corona.
Idadi ya watu ambao wamefariki kutokana na maambukizi ya virusi vya corona imefikia watu 35 818.
Nchini Ufaransa, watu 39 wamefariki ndani ya masaa 24 kutokana na maambukizi ya virusi vya corona huku idadi ya watu waliofariki ikitajwa kuwa watu 31 700.
0 Comments